Mwanamuziki Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu Burna Boy kutoka Nchini Nigeria ameshinda Tuzo ya Best International Act katika Tuzo za Muziki za BET Awards 2021 zilizotolewa usiku wa kuamkia leo nchini Marekani.

Burnaboy alikuwa akichuana na Diamond Platnumz , Wiz Kid, Ayana Kamura Emicida, Headie One, Young Tand Bugsey na Youssou Phamusik katika kipengele cha BEST INTERNATIONAL ACT 2021.

Hii inakuwa mara ya tatu kwa Burna Boy kushinda kipengele hicho kwani alishachukua tuzo tena mwaka 2019 na 2020.

Tuzo za BET rasmi zilianza kutolewa mwka 2001, zimeandaliwa mahususi kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo, zinatolewa usiku wa leo huko nchini Marekani.

Naibu Spika: Tuendelee kuwasaidia hawa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 28, 2021