Watoto watatu wa kike wenye ulemavu wa macho wamefariki Dunia kufuatia kutokea kwa ajali ya moto katika Bweni la kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi, uziwi na kutoona lililopo eneo la Buhangija Mkoani Shinyanga.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP. Janeth Magomi imesema moto huo ulitokea majira yaa saa mbili na nusu usiku wa Novemba 23,, 2022 metokea jana Novemba 23,2022 katika bweni lililokuwa na watoto 32.

Bweni lililoteketea kwa moto katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu, Buhangija, Shinyanga.

Amesema, “Polisi inafanya uchunguzi wa tukio la moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika ulioteketeza bweni la kituo cha kulelea watoto walemavu Buhangija cha Shinyanga mjini na kusababisha vifo vya watoto wakike watatu.”

Aidha, Kamanda Magomi amewataja waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Caren Mayenga (10), Niliam Limbu (12) na Catherine Paulo (10) ambao ni Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Buhangija.

Majaliwa ataka mkakati maeneo ya uwekezaji SGR
Rais Samia afungua mkutano EALS