Hatimaye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale umemalizika huku mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM), Zuberi Kuchauka akiibuka mshindi wa kiti cha ubunge.

Msimamizi wa uchaguzi Jimboni hapo, Luiza Mlelwa amesema kuwa waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 55777 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 40706 kura halali zilikuwa 40,301 kura zilizokataliwa ni 405

Akimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Liwale msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa, Zuberi ameshinda kwa kura 34, 582 sawa na asilimia 85.81

Aidha, mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge, Zuberi Kuchauka amesema kuwa ameyapokea matokeo hayo kwa furaha na ameahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Liwale kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Kuchauka amesema kuwa changamoto nyingi zilizopo katika Jimbo la Liwale ni pamoja na miundombinu ya Barabara, Maji, Elimu, Mawasiliano na Afya ambapo ameahidi wananchi kuwa atashughulikia changamoto hizo.

Kwa upande wake, Abdul Kombo Ngakolwa ambaye ni mgombea wa Chama cha (AAFP) chama cha wakulima amesema ameridhishwa na  ushindi  alioupata  mgombea wa (CCM) na amempongeza kwa ushindi huo.

“Mara zote mtu unaposhindana lazima mmoja ashinde, asiyekubali kushindwa siyo mshindani” amesema Kombo

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 15, 2018
Video: DataVision yashiriki mashindano ya Rotary Dar Marathon kuchangia huduma hospitali ya CCBRT

Comments

comments