Mgogoro baina ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), umemalizika baada ya jukwaa la wahariri nchini (TEF), kuwakutanisha viongozi wakuu wa taasisi hizo.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera, ameongoza kikao cha maridhiano baina ya pande hizo mbili kuhusu ushiriki wa TBC katika kuripoti kampeni za uchaguzi mkuu kwa wagombea wa CHADEMA.

Vyombo vya habari vya umma vimekumbushwa kutoa fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 53(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, sambamba na Maadili ya Uchaguzi na Katiba ya Tanzania

Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam, kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile.

Agosti 28, wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika viwanja vya Zakheim Mbagala jijini Dar es Salaam, Mbowe aliwafukuza waandishi wa TBC akiwatuhumu kukatisha mara kwa mara matangazo ya moja kwa moja (live).

Lissu ,Membe waungana
Majaliwa: Chama chetu hakikurupuki