Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza oparesheni mpya waliyoipa jana la ‘Kata Funua’ lenye lengo la kujiimarisha zaidi maeneo ya vijijini.

Oparesheni hiyo imetangazwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kusini, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Alieleza kuwa oparesheni hiyo ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kwa uchaguzi wa mwaka 2019/20 ambapo itatekelezwa kwa kufanya mikutano mingi maeneo ya vijijini.

“Ndugu zangu utajiri wa kwanza wa majimbo ni watu. Kwa kanda ya Kusini kuna watu wengi, lakini ina ardhi nzuri na yenye rutuba, jangwa kwa kusini na ukichanganya na idadi ya watu waliopo na fursa zilizopo, kanda hii inastahili kuwa kiongozi,” alisema Mbowe.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Edward Lowassa aliwataka viongozi hao kuzingatia umoja na mshikamano na kwamba mtu yeyote atakayetaka kuvuruga umoja ndani ya chama hicho achukuliwe hatua mara moja.

“Haya yanayotokea kwa wengine yasije yakatokea ndani ya chama chetu,” alisema Lowassa. “Tuyakatae na tushikamane tuwe kitu kimoja ili tuendelee kukijenga chama kwa sababu umoja ni kitu muhimu katika kupigania maendeleo,” aliongeza.

Viongozi hao walisisitiza kuwa kuweka misingi bora kuanzia ngazi za chini kutawasaidia kushinda kuanzia chaguzi za Serikali za mitaa mwaka 2019 na kuwa imara zaidi kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Dk. Bana adai uamuzi wa Ndalichako kuhusu Diploma ni dhambi ya ubaguzi
Jordi Alba Hatarini Kuikosa El Clasico