Chama Cha Wananchi (CUF) mkoa wa Kagera kimepanga kufanya maandamano kupinga kufanyika kwa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar uliopangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

Kaimu Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Kagera, Saverina Mwijage, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa watafanya maandamano hayo Jumatatu kwa lengo la kushinikiza serikali kutoendelea na uchaguzi huo wa marudio na kumtambua Maalim Seif Sharif Hamad kama mshindi halali wa uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

“Tumedhamiria kuandamana ili kumfikishia ujumbe wetu Rais John Magufuli kupitia kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongella lengo letu hasa ni kupinga uchaguzi wa Zanzibar. Hali ya Zanzibar kwa sasa haiko shwari, watu wanatishiwa maisha yao, wanaishi kwa hofu juu ya maisha,” Mwijage ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake (CUF-Taifa) anakaririwa.

Akieleza ratiba ya maandamano hayo, alisema kuwa yataanza majira ya saa nne kamili asubuhi na kuhitimishwa saa tisa kamili alasiri katika Uwanja wa Shujaa Mayunga mjini Bukoba ambapo utafanyika mkutano wa hadhara.

 

Video Mpya: Nay wa Mitego - Shika Adabu Yako
Zitto ampa hili Magufuli... ashindilia msumari wanaokwepa mali, madeni yao kuonekana