Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Benjamin Zakaria, Mkazi wa Tungi, amenaswa akiwa ndani ya chumba cha watu mahututi (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro akijifanya kuwa daktari.

Zakaria ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kitabibu anadaiwa kuingia katika wodi kadhaa na kufanya mazungumzo na wagonjwa kabla hajabainika alipokuwa akiwahoji wagonjwa mahututi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa mtu huyo alikamatwa baada ya kutiliwa shaka na muuguzi mmoja ndani ya ICU, ambaye aliamua kumhoji maswali ya kitabibu yaliyokosa majibu.

Kamanda Matei alisema kuwa muuguzi huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa Hosptali hiyo, ambao uliwasiliana na Jeshi la Polisi lililomtia mbaroni kwa hatua za kisheria.

Daktari Feki akiwa mikononi mwa Polisi

Daktari Feki akiwa mikononi mwa Polisi

“Muuguzi huyo aliyemtilia shaka aliufahamisha uongozi wa hospitali hiyo ambao uliripoti Polisi na kufanikiwa kumkamata, alisema Kamanda Mtei.

Mtu huyo aliyejifanya kuwa mkaguzi kutoka nje ya hospitali hiyo aliyetaka kujua hali ya huduma wanazopewa wagonjwa, alijinasibu kuwa yeye aliwahi kuwa askari wa Jeshi na alikuwa tabibu hivyo anayo ruhusa ya kuingia mahali popote na kutoa huduma.

Magazeti: Gwajima Alivyoingia kwenye 18 za Polisi, Wabunge Chadema Wapanga Kugoma
Daraja la Nyerere lakusanya Bilioni za wenye magari, pikipiki, bajaji