Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imefanikiwa kukamata kilo 88.27 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine zikiwa ndani ya gari aina ya Toyota Prado iliyokuwa imetelekezwa barabarani eneo la Kimara Korogwe Mkoani Dar es salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam , Kamishina Jenerali Gerald Kusaya amesema, dawa hizo zimekamatwa Juni 2 mwaka huu , saa saba usiku katika eneo la Kimara Korogwe.

”Dereva wa gari hilo baada ya kugundua anafuatiliwa alianza kulizugusha gari hilo katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Kinondoni na hatimaye kutokana na maofisa wa taasisi hiyo kuwa wamejipanga alikamatwa maeneo ya Kimara Korogwe akiwa amelitelekea gari kabla ya kuwatoroka maofisa hao.

”Pakti 12 za dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilo 12.25 pamoja na kontena za plastiki 73 ndani yake kukiwa na dawa za kulevya aina ya Methaphetamine zilizo na uzito wa kilo 76.02,”amesema Kamishna Kusaya.

Aidha Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya kwa sasa inaendelea na upepelezi wa  kuwasaka wahusika wanaohusika na dawa hizo ikiwemo mmiliki wa gari.

Ametoa wito kwa wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya waache mara moja kwa kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama iko macho, haijalala

Meneja Simba SC afichua siri
Mgongolwa atoa afafanua uchaguzi TFF