Mkuu wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha Nurdin Babu ametoa agizo kwa Halmashauri ya Longido kutenga fedha kipindi Cha kupanga Bajeti kwa ajili ya kuendeshea Mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo).

Amesema hayo wakati akihitimisha mafunzo ya jeshi la akiba yaliyochukua takribani miezi minne katika Kata ya Engarenaibor.

Ameeleza kuwa jeshi linahitaji watu wenye nidhamu na weledi,nakuwahasa kutokubali kushawishiwa na watu wenye Nia ovyu kwa sababu wamewaona wamepata mafunzo mazuri. 

“Askari  hawa ni wa halmashauri, hivyo mtakavyoanza kutenga bajeti mwakani mwezi wa pili ,tengeni fungu la jeshi la akiba” amesema Babu.

“Mmejifunza kushika silaha ,pamoja na jinsi ya kufunga na kufungua silaha  na mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Uhamiaji,TAKUKURU,Usalama wa raina hata usalama wa Taifa hivyo mmeongeza ujuzi,mkawe wazalendo kwa nchi yetu” ameeleza Babu.

Diamond, Ali Kiba, Zuchu na Harmonize Waongoza
Uswizi yaidhinisha Kifaa cha kujiua