Hatimae klabu ya Manchester City imetoa taarifa rasmi kuhusu kiungo wao kutoka nchini Ubelgiji Kevin De Bruyne, ambaye alipatwa na majeraha ya goti akiwa katika maandalizi ya mchezo wa mzunguuko wa pili wa ligi kuu msimu huu ambao utawakutanisha na dhidi ya Huddersfield Town mwishoni mwa juma hili.

Manchester City wamethibitisha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu, sawa na majuma 12.

Baada ya kufanyiwa vipimo, imebainika Kevin De Bruyne amepatwa na majeraha makubwa eneo la goti lake la mguu wa kushoto, lakini hatofanyiwa upasuaji, kama ilivyokua ikielezwa hapo awali.

De Bruyne ametonesha eneo alilowahi kupata jeraha wakati akiwa katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi uliowakutanisha dhidi ya  Everton mwaka 2016.

Mwishoni mwa juma lililopita alikua sehemu ya kikosi cha Man City, kilichochomoza na ushindi wa maboa mawili kwa sifuri dhidi ya Arsenal, akitumika kama mchezaji wa akiba.

Msimu uliopoita De Bruyne alifanikiwa kufunga mabao manane na kutoa pasi za mwisho 16, na kutoa mchango wa klabu ya Man City kufikisha alama 100 kwenye msimamo wa ligi ya England, huku wakitwaa ubingwa kwa mara ya kwanza chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Hispania Pep Guardiola.

MICHEZO AMBAYO KIUNGO HUYO ATAIKOSA.

Agosti 25: Wolverhampton Wanderers (Ugenini)

Septemba 1: Newcastle United (Nyumbani)

Septemba 15: Fulham (Nyumbani)

Septemba 18/19: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi.

Septemba 22: Cardiff (Ugenini)

Septemba 29: Brighton (Nyumbani)

Oktoba 2/3: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi

Oktoba 7: Liverpool (Ugenini)

Endapo itamchukua muda wa miezi mitatu kabla ya kurejea kikosini, De Bruyne atakosa mchezo mingine sita ambayo ni.

Oktoba 20: Burnley (Nyumbani)

Oktoba 23/24: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi

Oktoba 28: Tottenham (Ugenini)

Novemba 3: Southampton (Nyumbani)

Novemba 6/7: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi

Novemba 11: Manchester United (Nyumbani)

Claudio Marchisio aondoka Juventus FC
Kangi Lugola aagiza kukamatwa kwa wanafunzi watoro