Hatimaye mshindi wa tuzo ya MTV/MAMA, Diamond Platinumz amekamilisha kurekodi wimbo wake na mkali wa RnB toka Marekani, Ne-yo.

Collabo hiyo imefanywa kwa ushirikiano na mtayarishaji wa Tanzania, Sheddy Clever ambapo Diamond amesifia kazi nzima iliyofanywa akiitabiria kuwa ‘hit song’ ya kimataifa.

“Thanks alot my Brother @neyo and the Whole Compound Crew had a great Session, and it was realy nice working with you…can’t wait for the World to hear this Hit Song!! @Diamondplatnumz ft @neyo ….. Cc @sheddyclever @Compoundu @thecorpshow @Jullianl #AfricaTotheWorld,” Diamond aliandika kwenye post ya Instagram ikiwa na picha inayoonesha kazi ilivyofanyika.

Ne-yo ambaye amekuja Afrika Mashariki kushiriki msimu wa tatu wa Coke Studio Africa amefanya collabo na wasanii wawili wakubwa Tanzania, Diamond na Ali Kiba.

Comments

comments