Diamond ameonekana kulipa fadhila kwa Alikiba baada ya kumuombea mashabiki wampigie kura kwenye tuzo ya MTVEMA 2016, akiwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki anayewania tuzo hiyo.

Wengine  wakiwemo Wizkid na Olamide wa Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini huku mshindi katika hatua ya kwanza ataendelea kwenda kuwania kipengele cha Worldwide Act: Africa/India ambacho mwaka jana alishinda Diamond Platnumz.

Akiongea kwenye kipindi cha D’Wikend Chatshow cha Clouds TV,amesema, “Nimesikia Alikiba amechaguliwa kwenye tuzo za MTV EMA. Tufute zile zama za kusema kwasababu wewe unam-support Diamond ndio huwezi kumpigia kura Alikiba. Akikosa tuzo hiyo haiji kabisa Tanzania na itaonekana watanzania wote tumeikosa. Kwahiyo tuhakikishe tuna VOTE ili tuirudishe tuzo hiyo nyumbani.”

Video: Jaji Mutungi anaivuruga CUF - Mbowe
Chadema watangaza staili mpya ya Ukuta, sasa ni mwendo wa ‘kupaa’