Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake.

Siku moja baada ya DW kuitaja ngoma aliyoshirikishwa na marehemu Papa Wemba, Pour Soi kuwa imefunga mwaka kwa kuwa namba moja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kidogo aliyowashirikisha P-Square nayo imefunga mwaka kwa kishindo.

Wimbo huo umekuwa wimbo wa mwaka katika kituo cha redio cha Radio Afro cha Australia, baada ya kuzishinda nyimbo za magwiji wengi wa Afrika wakiwemo Wizkid, Davido, Tiwa Savage, Iyanya na wengine kibao.

Obama awafungashia virago wanadiplomasia wa Urusi
Ubabe wa Faru John na kuwapanda wanae vyatajwa kumgharimu, Maghembe anena