Hatimaye Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Joyce Ndalichako ameagiza Baraza la Mitihani nchini (NECTA) kufuta mfumo wa upangaji wa matokeo wa GPA.

Dk. Ndalichako ameitaka NECTA kurudisha mfumo wa upangaji matokeo uliokuwa ukitumika awali wa kutumia ‘Division’.

Waziri huyo wa elimu amesema kuwa amechukua uamuzi huo baada ya NECTA kushindwa kumpa sababu za kisayansi zilizopelekea kubadili mfumo wa kupanga matokeo, kama alivyokuwa amewataka kufanya hivyo awali.

Wadau wa elimu waliwakuwa wakiulalamikia mfumo huo wa GPA kuwa ulishindwa kupima vyema ufaulu wa mwanafunzi wa sekondari.

Juma Nature: Msishangae kusikia nimefanya kazi na Snoop Dogg
Bifu Jipya: Rick Ross amchana Birdman kuhusu Lil Wayne