Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Zimbabwe ambaye pia ni Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Generali (Mstaafu) Constantino Chiwenga, yaliofanyika Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema Tanzania inathamini urafiki wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili ambao umekuwepo tangu enzi zaharakati za Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, na kuongeza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kukuza zaidi ushirikiano uliopo pamoja na kuungana na nchi hiyo kupinga vikwazo mbalimbali vinavyoikabili.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Makamu wa Rais Zimbabwe ambaye
pia ni Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mheshimiwa Generali (Mstaafu), Constantino Chiwenga,Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam.

Kwa Upande wake Makamu wa Rais Zimbabwe, Generali (Mstaafu), Constantino Chiwenga amesema Tanzania ni nchi ambayo imetoa mchango mkubwa kwa Zimbabwe na nchi za Kusini Mwa Afrika katika harakati za ukombozi ambao kamwe hautosahaulika.

Amesema kwa sasa mataifa haya yanapaswa kujielekeza zaidi katika ushirikianio wa kiuchumi kwa kuwafanya wananchi wake kutumia fursa ya ushirikiano uliopo kukuza uchumi wao na
kujiletea maendeleo na kurithisha ushirikiano huo vizazi na vizazi.

Simba SC yafafanua alipo Juma Mgunda
SportPesa: Tulijadiliana na Young Africans