Shirikisho la soka Duniani (FIFA ) limefungua kesi dhidi ya Argentina baada ya mlinda mlango Emiliano Martinez kuonesha ‘tabia ya kukera’ baada ya ushindi katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa nchini Qatar Desemba 2022.

Baraza la FIFA linalosimamia michezo limeanzisha uchunguzi baada ya ishara kadhaa za Martinez ambazo zimetafsiriwa kuwa ni chafu akiwa na tuzo ya golikipa Bora wa mashindano (Golden Glove).

FIFA imesema kesi hiyo inahusu ukiukwaji wa kifungu cha 11 (tabia ya kukera na ukiukaji wa kanuni za uchezaji wa haki) na kifungu cha 12 (utovu wa nidhamu wa wachezaji na viongozi).

Mlinda mlango wa Aston Villa Emiliano Martinez ambaye alikuwa shujaa katika mikwaju ya penati kufuatia sare ya 3-3, alipewa kadi ya njano kwa kwa vitimbi vyake wakati wa mikwaju ya penati, na kuendelea baada ya mchezo kumalizika.

Ishara yake ya kutwaa taji la Golden Glove kabla ya Kombe la Dunia kukabidhiwa ilienea kwa kasi, na aliendelea kumkejeli Kylian Mbappe wa Paris Saint-Germain katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo, na pia wakati wa Gwaride baada ya kurejea nyumbani kwao Argentina.

Sambamba na Argentina, Croatia pia wanachunguzwa kwa makosa ya ‘ubaguzi’ kufuatia baadhi ya wachezaji kuimba wimbo wenye sauti ya chini ya kifashisti baada ya ushindi wao wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Morocco.

Beki Dejan Lovren alilazimika kukana madai hayo na kusema wimbo huo haukuwa na uhusiano wowote na ufashisti na kudi ni upotoshaji usiofaa.

“Kwangu mimi, ni wimbo wa kizalendo kuhusu nchi yangu, ambayo inamaanisha kuwa ninaipenda nchi yangu.” amesema Lovren

Hata hivyo, FIFA imefungua uchunguzi kuhusu ‘ukiukaji unaowezekana wa vifungu 13 (ubaguzi) na 16 cha kanuni za nidhamu za FIFA.

Mataifa mengine matatu ya Kombe la Dunia pia yamewekewa vikwazo, huku Serbia, Ecuador na vyama vya soka vya Mexico vikitozwa faini kwa nyimbo zilizoimbwa na wafuasi wao.

Habib Kyombo: Kocha ameniamini, sijamuangusha
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 16, 2023