Aliyekua daktari wa klabu ya Chelsea, Eva Carneiro amemtaka meneja wa zamani wa klabu hiyo, José Mourinho, akimuomba radii hadharani.

Eva amefikia uamuzi huo baada ya madai kwamba Mourinho alimdhalilisha na kumuita ni mtu wa hovyo hovyo baada ya kuingia kumtibu kiungo Eden Hazard katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huu dhidi ya Swansea City.

Eva aliamua kuondoka moja kwa moja Chelsea licha ya Mourinho aliyekuwa amemsimamisha kwa muda kukubali arejee.

Baada ya halo akafungua kesi ambayo inaonekana kukosa nguvu kwa namna ya kutaka kulipwa, lakini suala la kuomba radhi linawezekana na wanasheria wake wameonekana kutaka kulisimamia jambo hilo.

Wakati Eva anaingia kumtibu Hazard, matokeo yalikuwa ni bao 1-1, jambo ambalo Mourinho aliona kama hatua hiyo ilikuwa akipoteza muda na wao walikuwa wakicheza vizuri na wangeweza kusawazisha.

Arsenal Watinga Robo Fainali
Real Madrid Watangulia Robo Fainali