Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo amesema kuwa Serikali haijazuia kufanya mikutano hotelini au kwa watumishi wake kualala kwenye hoteli zinazao milikiwa na sekta binafsi badala yake imezuia matumizi makubwa ya fedha za Serikali.

Amsema hayo alipokwa akijibu swali la Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro, aliyemtaka Rais Magufuli kufungua milango kwa taasisi za Serikali na Wizara  zake kutumia hoteli za watu binafsi katika shughuli zake za mikutano ili kuwezesha wamilki hao kujiendesha kwa faida na kulipa kodi Serikalini.

“Watu wamekuwa wakitafsiri  tofauti kauli ya Rais Magufuli, ukweli ni kwamba yeye hakuzuia watumishi wa Serikali kufanya mikutano ama kulala kwenye hotel za kifahari, alichosema ni kwamba hataki matumizi makubwa ya fedha za Serikali yasiyo  na ulazima”amesema Gambo.

Aidha, Gambo amewataka  watu kuacha kunukuu vibaya kauli za Rais Magufuli kwa lengo la kujipatia umaarufu, badala yake wazingatie maelekezo sahihi yanayotolewa na Serikali ambayo yana nia njema  ya kubana matumizi na kuinua uchumi wa nchi.

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Ikulu
Majaliwa aagiza jeshi la polisi kuwasaka waliofanya mauaji bagamoyo