Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres amelaani mashambulio yaliyotekelezwa na watu waliojihami wasiojulikana katika kijiji cha Tchombangou na Zaroumbareye, eneo la Tillabéri nchini Niger.

Guteress, ameelezea rambi rambi zake kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na serikali ya Niger na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Guterres anatumai kwamba mamlaka Niger watafanya kila wawezalo kuwafikisha mbele ya sheria watekelezaji wa kitendo hicho cha kinyama huku wakiimarisha ulinzi wa raia.

Guterres amesisitiza umoja na msaada wa Umoja wa Mataifa kwa serikali na watu wa Niger katika vita dhidi ya ugaidi, misimamo mikali na uhalifu wa kupangwa.

TCRA yaifungia Wasafi TV
Januari 6 mwisho wa kukata tiketi kwa mkono