Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara imezungumzia suala ujenzi wa halmshauri ya Tarime Vijiji Mkoani Mara kujengwa eneo ya Nyamwaga ili kuhudumia wananchi kwa ukaribu.
 
Amesema kuwa kuhusu ombi hilo serikali haina kipingamizi na pia ameagizwa na Waziri mkuu kushughulikia suala hilo ikiwa ni pamoja na kukagua eneo la kujengwa ili kujiridhisha kama wananachi hawatataka fidia kwenye eneo lililotolewa na serikali ya kijiji cha Nyamwaga ili kujenga Halmashauri hiyo.
 
“Serikali haina fedha za kutoa fidia pia Halmshauri ikijengwa apa itahudumia wananachi wa kata zote 26 pia Waziri Mkuu alipita hapa amenituma kwamba nikipeleka muhutasari huu na eneo mmetoa bure niandike na mapendekezo yangu Mh. Waziri amesema kuwa serikali haina kipingamizi chochote kuhusu halmashauri ya Tarime vijijini kujengwa Nyamwaga,” amesema Waitara.
 
Aidha, Serikali ya kijiji cha Nyamwaga ambapo Halmashauri hiyo inatarajiwa kujengwa imetoa eneo bure hekari 128 ili serikali iweze kujengwa hapo kwa lengo la kusogeza huduma za jamii karibu.
 
Vile vile Waziri amezungumzia suala la Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima kuhamisha Fedha za Ruzuku zilizokuwa zinatolewa na Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu Nyamongo kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo kuwa sasa zitaenda kufanya shughuli za Maendeleo katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara ambapo serikali imesema kuwa suala hili haliwezekani bali fedha zitaendelea kutumika vyema kama Halmashauri ilivyokuwa ikifanya awali bali zitasimamiwa moja kwa moja na ofisi ya TAMISEMI.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 2, 2019
Waitara aagiza serikali ya kijiji kutumia fedha milioni mianane