Edward Moringe Sokoine ni kati ya viongozi bora walioonekana kuwa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu, akifuatilia utendaji kazi na kukemea ulaji Rushwa na ubadhilifu wa mali za Umma.
Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980, na tarehe 24 Februari 1983 hadi alipofariki katika ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha Bunge Dodoma kuelekea Dar es salaam.

Gari lilivyoharibika baada ya ajali iliyomuua Edward Sokoine
Kifo cha Sokoine kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.
Uadilifu wake na uchapa kazi umepelekea hadi Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro kupewa jina la ‘Chuo cha Kilimo cha Sokoine’ ambacho hadi sasa kinaitwa Chuo Kikuu cha Sokoine.