Kumekuwa na changamoto ya majengo kukosa ubora hali inayosababisha kushindwa kudumu kwa muda mrefu licha ya kujengwa kwa gharama kubwa.

Hali hii imetokana na ukosefu wa maandalizi ya kitaalamu pamoja usimamizi mzuri wakati wa ujenzi wake, jambo linalotoa fursa kwa baadhi ya wakandarasi wasio waaminifu kutumia mwanya huo kujenga majengo yaliyokosa ubora na kusababisha hasara kwa wamiliki.

Wakala wa majengo Tanzania (TBA) moja kati ya majukumu yake ni kuandaa ramani za ujenzi na kusimamia ubora unaotakiwa kwa majengo ya huduma na makazi hapa nchini.

Kaimu meneja wa mawasiliano na masoko wa TBA Fredrick Kalinga amesema umefika wakati sasa kwa watanzania na wawekezaji kufanya kazi na TBA ili kuwa na uhakika wa majengo bora ya uhakika kwa shughuli mbalimbali ili kuepuka hasara na maafa yanayoweza kusababishwa na ujenzi usiozingatia ubora.

Amesema TBA inawabunifu na wataalamu wa ujenzi wa majengo ya aina zote huku wakiaminiwa katika ukarabati wa majengo muhimu ya umma.

Wakala wa majengo Tanzania pia wanauza nyumba walizojenga katika mradi mkubwa wa nyumba- Bunju.

TBA ni taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuongeza ubora wa utoaji huduma kwa kutumia njia za kibiashara na uongozi bora wa fedha ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kupunguza gharama za uendeshaji , huduma bora ya makazi kwa Serikali na nyumba za gharama nafuu kwa Watumishi wa Umma na pia kutoa huduma bora ya Ushauri wa kwa Serikali.

Siri ya sentensi ''Kupanga ni Kuchagua''
Diamond Platnumz atoa pole waathirika ajali ya moto, aahidi kuwafuta machozi