Viongozi wakuu wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), wamefanya mazungumzo kujadili hatma ya Rais Cyril Ramaphosa anayekabiliwa na shinikizo la kisiasa linaloweza kumwondoa madarakani.

Rais Ramaphosa, ni miongoni mwa wale wanaoshiriki majadiliano hayo yanayofanyika siku moja kabla ya bunge kupiga kura inayoweza kuanzisha mchakato wa kumtoa mamlakani.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Picha ya News 24.

Kiongozi huyo, anaandamwa na kiwingu cha madai ya kukiuka katiba baada ya jopo maalum la uchunguzi kuchapisha ripoti iliyomtuhumu kuficha taarifa za wizi wa maelfu ya dola uliotokea kwenye shamba lake binafsi.

Desemba 5, 2022 Rais Ramphosa alisema hatojiuzulu kutokana na kashfa hiyo iliyokigawa chama cha ANC kuelekea mkutano mkuu wa chama katikati mwa mwezi Disemba.

262 jela miaka miwili kwa kuandamana
Cruiser yagonga gari la Jeshi, watatu wafariki