Wacheza tenesi waingereza Heather Watson na Naomi Brady kwa pamoja wametupwa nje ya michuano ya Luxembourg Open katika hatua ya robo fainali.

Naomi Broady amechapwa na Monica Puig wa Puerto Rico kwa seti 6-0 5-7 6-1 wakati Watson ambaye ni mchezaji namba mbili kwa ubora nchini Uingereza namba 81 duniani amepoteza kwa seti 6-4 6-4 mbele ya Elise Mertens wa Ubelgiji.

Puig atakutana na Elise Mertens katika hatua ya nusu fainali na Pauline Parmentier wa Ufaransa atacheza na Caroline Witthoft wa Ujerumani.

Fainali ya michuano hiyo ya Luxemberg Open itapigwa tarehe 21 mwezi Oktoba.

 

Video: Lissu awaibua Nape, Ridhiwani, Wamebana wameachia
Korea Kaskazini yaitumia barua Australia