Saa chache kabla ya kuapishwa kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameanza kupokea salamu za pongezi kutoka kwa viongozi wa mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Rais Kagame amemuandikia Rais huyo mteule wa Tanzania ujumbe wa pongezi huku akimhakikishia kuwa ataendelea kudumisha urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

“Kufuatia kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kukutumia salamu za dhati, pongezi na heri. Hii ni kwa niaba yangu mwenyewe, serikali yangu na watu wa Rwanda. Napenda pia kutumia nafasi hii kukuhakikishia msimamo wetu wa kudumisha na kuimarisha msimamo wa kirafiki kwa ushirikiano kati ya mataifa yetu mawili na watu wake.”

Rais Kagame atatarajiwa kuwa mmoja kati ya viongozi wa nchi mbalimbali watakaohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Dkt. Magufuli kuwa rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndoa Ya Siri Ya Wema Sepetu Yapata Maelezo Ya Mhusika
Hashim Rungwe Atimkia Mahakamani Kuhusu Uchaguzi Wa Rais