Kaimu Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Hitimana Thiery, amewataka Mashabiki na Wanachama wa klabu huyo kusahau yaliopita na kuganga yajayo.

Hitimana ametoa rai hiyo kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, saa kadhaa zikisalia kabla ya kikosi chake kushuka dimbani kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha huyo kutoka nchini Rwanda amesema kilichotokea ni sehemu ya matokeo ya mchezo wa soka, na kuna haja ya kila mmoja wao kuamini hivyo.

“Kilichotokea ni sehemu ya SOKA kwa sasa tunasonga mbele kuna michuano mingine ipo mbele yetu. Tulienda kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye ligi kwahiyo tunapaswa kuelekea nguvu na akili zetu huku.”

“Kuelekea mchezo wetu wa leo dhidi ya Polisi Tanzania wachezaji wapo tayari, tulipata siku mbili za maandalizi na kila kitu kimeenda sawa.” amesema Hitimana Thiery.

Kocha Hitimana atakiongoza kikosi cha Simba SC kama Kaimu Kocha Mkuu kwa mara ya kwanza leo Jumatano (Oktoba 27), kufuatia Kocha Didier Gomes kufikia makubaliano na uongozi ya kusitisha mkataba wake tangu jana Jumanne (Oktoba 26).

Simba SC yenye alama 4 zinazoiweka katika nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu, inakutana na Polisi Tanzania iliyo kileleni kwa kufikisha alama 9.

Manara amuhofia Prince Dube
Manara afichua siri Simba SC kufungwa