Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa serikali iliweka uwepo wa tozo za uzalendo kwenye miamala ya simu kwa lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia katika ujenzi wa barabara vijijini pamoja na upatikanaji wa huduma za maji katika maeneo hayo.

Amesema hayo leo Julai 27, 2021, Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwaapisha mabalozi 13 wa nchi mbalimbali aliowateua siku za nyuma ambapo amesema Julai 29 mwaka huu atapokea maoni ya kamati aliyoiunda kuhusu miamala ya simu.

Rais Samia amesema sehemu kubwa ya fedha ya makato ya miamala ya simu yatakwenda kujenga njia za vijijini lengo likiwa kuwasaidia wamamchi ambao wamewekeza katika kilima huku barabara za vijijini zikiwa si rafiki kwao.

Makato haya tuliyaweka kwa nia njema tu nchi yetu sasa hivi wakulima wameamka na kilimo kikubwa lakini wakivuna wanashindwa kuyaleta mavuno kwenye masoko tatizo ni njia kwa hiyo sehemu kubwa ya pesa hii itakwenda kwenye kujenga njia za vijijini, tumesikia vilio vya Watanzania, tozo zipo ila tutaangalia njia nzuri ambayo haitaumiza watu, serikali ipate na maendeleo yaendelee,” amesema Rais Samia.

Young Africans, Azam FC zaangukia Kundi B, C
Pro. Ndalichako azitaka taasisi za sayansi kufanya tafiti