Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi inazizidi kuongezeka ambapo mpaka sasa watu takribani kumi na moja wanasemekana wamefariki katika tetemeko hilo lililotokea jana katika mikoa ya kanda ya ziwa,Viongozi mbalimbali wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wamesema watu zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika tetemeko hilo lililo ukumba ukanda huo.

Wafanyakazi wa kutoa huduma za misaada wamesema watu kadhaa bado wako chini ya vifusi baada ya majengo mbalimbali kuporomoka katika sehemu tofauti tofauti za mikoa hiyo,na kudaiwa kuwa hospitali nyingi katika maeneo hayo zimejaa majeruhi wengi. tetemeko lilitokea linasemekana kuwa ndilo tetemeko kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Tanzania.

 

Mapambano Kati ya Waasi Na Serikali Yazidi Kupamba Moto Nchini Syria
Chidi Benzi Arudi Tena Kwenye Madawa Ya Kulevya