Umoja wa Mataifa, umesema unakadiria kwamba idadi ya wakazi duniani itafikia bilioni nane kufikia Novemba 15, 2022 na itaendelea kukua ingawa kwa kasi ndogo na kwa tofauti ya kimaeneo, katika miongo ijayo.

Makadirio hayo, ni mara tatu zaidi kuliko wakazi bilioni 2.5 waliohesabiwa mwaka 1950 ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya wakazi duniani limesema licha ya kuongezeka kwa watu hao, katika miaka ya 1960, kasi ya kukua kwa idadi ya wakazi duniani imepungua kwa kiwango kikubwa.

Kupitia mmoja wa maafisa wake, Rachel Snow amesema kupungua kwa watu hao kunatokana na majanga mengi ya kivita, mafuriko, ikiwemo na magonjwa kama janga la Uviko-19 ambalo liliondoka na maisha ya watu wengi Duniani.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 8, 2022 
Aliyepigwa risasi kwenye kampeni asema anaanzia alipoishia