Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu, ameitaka jamii kuwatambua wafungwa na mahabusu kama sehemu ya jamii kwa kuwatembelea na kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali yatakayosaidia kutatua changamoto zao.

Dkt. Jingu ameyasema hayo akiwa katika Gereza Kuu la Isanga Jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake katika Magereza mbalimbali nchini yenye lengo la kusikiliza wafungwa na mahabusu hususani wenye changamoto zinazohusu masuala ya Ustawi wa Jamii.

“Wafungwa hawa wametokana na jamii inayotuzunguka hivyo hatuna budi kuwasikiliza na sisi tumesikia changamoto zao tunakwenda kuzifanyia kazi na nyingine zilizo nje ya uwezo wetu tutashirikiana na wenzetu Serikalini tuone namna ya kuzitatua,” Amesema Dkt. Jingu.

Aidha Dkt Jingu amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri wanayoifanya kuhakikisha mahabusu na wafungwa magerezani wanapata usimamizi mzuri na kutatuliwa changamoto zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza Kuu la Isanga, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Fumbuka Ikobela, amesema ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Jingu ni faraja kwao kwani ni hatua muhimu ya kufikisha changamoto zinazowakabili mahabusu na wafungwa na kufanyiwa kazi.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu la Isanga, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Fumbuka Ikobela mara baada ya kuwasili katika gereza hilo jijini Dodoma yenye lengo la kusikiliza wafungwa na mahabusu hususani wenye changamoto hasa zinazohusu masuala ya Ustawi wa Jamii.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma katika ziara yake yenye lengo la kusikiliza wafungwa na mahabusu hususani wenye changamoto hasa zinazohusu masuala ya Ustawi wa Jamii.

John Bocco amsikitisha Kim Poulsen
Kim Poulsen afichua siri ya ushindi dhidi ya Madagascar