Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli ametaka kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM na kuwataka viongozi watakaochaguliwa kuhakiki miradi yote ya umoja huo kuanzia ngazi ya chini.

Ameyasema wakati akifungua Mkutano wa tisa wa Jumuiya hiyo ambao ajenda yake kuu ni kufanya uchaguzi wa viongozi.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania, amesema kuwa miradi ya UVCCM mapato yake yamekuwa hayajulikani yanapoenda hivyo inahitaji kuhakikiwa na kuwekwa pamoja ili kuweza kuleta tija kwa umoja huo.

Rais Dkt. Magufuli pia amewataka UVCCM kuchagua viongozi wanaofaa na wanaoichukia rushwa ili waweze kuisaidia serikali badala ya kuwa viongozi wa kuyumbishwa na misimamo ya watu wenye pesa hali iliyofanya umoja huo kukosa muelekeo hasa kipindi cha uchaguzi.

Hata hivyo, Katika mkutano huo wanachama wapya waliojiunga na chama hicho hivi karibuni kutoka vyama mbalimbali vya upinzani waliwataka vijana wa CCM kuwa mstari wa mbele kuisaidia serikali.

Japan, Marekani na Korea ya Kusini kusaka njia za kujihami
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 11, 2017