Kocha mkuu wa Mwadui Jamhuri Kihwelo, amewatupia lawama mwamuzi wa mechi ya Ligi Kuu kati ya timu yake na Yanga, Selemani Kinugani, na washika vibendera Khalfan Sika na Haji Mwalukuta kwa kuchezesha mchezo huo kwa upendeleo kwa wapinzani wao.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo jana, Mwadui ilikubali kipigo cha mabao 2-1. Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, Julio alisema waamuzi walichezesha kwa maagizo maalum ya kuibeba Yanga.

Nataka muwe wakweli. Tusiwe na falsafa ya lazima bingwa awe Simba, Yanga au Azam. Mpira wa hivyo hakuna. Siku zote Yanga wakicheza Taifa kama kadi nyekundu haikutoka basi lazima itatokea penati ilimradi timu fulani ifungwe.

Kadi nyekundu ambayo mwamuzi katoa isiyokuwa na lazima. Kibendera alikuja na maagizo kabisa. Hakuwa anachezesha kwa usawa.

Kama angechezesha kwa haki, mpira huu hata kama tungecheza kwa dakika 300 Yanga wasingetufunga

Katika pambano hilo mlinzi wa Mwadui, Iddy Mobby alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya Donald Ngoma mnamo dakika ya 71.

Yanga walifanikiwa kutumia vizuri upungufu wa Mwadui uwanjani kupata bao la ushindi kupitia kwa kiungo wao Haruna Niyonzima dakika tatu kabla ya muda wa kawaida kutimia.

Cantona Apindisha Kauli Kuhusu Ajira Yake Olympique Marseille
Lugumi atoroka nchini usiku wa manane kukwepa rungu la Magufuli