Rapa na Kiongozi wa Kikosi cha Mizinga, Kala Pina ameukosoa wimbo mpya wa rapa mwenzake, Chid Benz ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond, wimbo ulioashiria ujio mpya wa rapa huyo baada ya msoto wa athari za dawa za kulevya.

Akiongea na Ladha3600 ya E-FM, Kala Pina alieleza kuwa Chid Benz amewaangusha mashabiki kwa ujio wake kwani walikuwa wanasubiri kumsikia rapa ‘anayekaza’ kama ilivyokuwa awali.

“Amewaangusha mashabiki… watu walitegemea kuja na kishindo cha kukaza. Tulitegemea angezungumzia maisha yake, kuhusu kutoka kwenye madawa na vitu kama hivyo…. Lakini wanaweza kuona kama imekuwa miyeyusho,” alisema Kala Pina.

Chid Benz na Ray

Kala Pina alisema kuwa kwa jinsi anavyomfahamu Chid Benz kama rapa mkali, katika wimbo huo bado hakuonesha uwezo wake kwa kiwango cha alichonacho.

Alimshauri Chid kuendeleza mtindo ambao watu walikuwa wanajua anafanya tangu zamani na wakamkubali.

Katika hatua nyingine, Kala Pina alimpongeza Chid kwa kufanikiwa kuachana na dawa za kulevya kurudi upya kwenye ‘hip hop’ akiwa kama kichwa chenya uwezo mkubwa na kinachoaminika kwenye muziki huo.

Lamine Kone Aomba Kuondoka Stadium Of Light
Kigwangalla alitangazia kibano shirika la LGBT linalohamasisha Ushoga