Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda amefanya ziara ya kikazi katika Kanda mbalimbali kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa kwa kusimamiwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Kamishna Nyanda amesema ameridhishwa na utekelezaji wake na kuwataka wakandarasi kumilisha ujenzi wa miradi hiyo kabla ya tarehe iliyopangwa ya ni Septemba 31, 2022.

Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda, akipokea maelekezo wakati wa ukaguzi wa miradi ya kanda inayosimamiwa na TAWA.

Akiwa katika Kanda ya Ziwa, Kamishna Nyanda alikagua miradi ya ujenzi wa barabara, lango la kuingilia wageni na camping site inayotekelezwa katika Pori la Akiba Kijereshi.

Katika Pori la Akiba Maswa, alikagua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 200, ukarabati wa kiwanja cha ndege Buruti, ukarabati wa kiwanja cha ndege Mbono, ujenzi wa kituo cha Askari, ujenzi wa ofisi pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya kudumu vya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu katika vijiji vya Malwilo (Meatu) na Lugalombogo (Itilima).

Moja ya miradi inayosimamiwa na TAWA ambayo imetembelewa katika ukaguzi uliofanywa na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda.

Kadhalika katika Kanda ya Magharibi, Kamishna Nyanda alikagua ujenzi wa jengo la kutoa habari (Information Center), lililopo katika Bustani ya wanyamapori Tabora (Tabora Zoo), na katika Kanda ya Kati na Nyanda za Juu Kusini alikagua ujenzi wa vituo vya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu vya Mtera na Mboliboli.

Ziara hiyo ya siku tano imefanyika Septemba 12 hadi 17, 2022, imefanyika katika Kanda tofauti za Ziwa Victoria, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati na Kanda ya nyanda za juu kusini ikihusisha miradi inayojengwa kwa kupitia Fedha za Maendeleo na Ustawi wa Taifa, mapambano dhidi ya Uviko-19 na fedha za bajeti ya kawaida.

Umeme Kigoma: Serikali kuokoa Bil 22.4
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 19, 2022