Baada ya kuambulia sare ya 3-3 dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Young Africans Cedrick Kaze amesema hana wa kumlaumu zaidi ya kuheshimu kilichotokea ndani ya dakika 90 za mpambano huo, uliochezwa jana Jumatano (Februari 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Kaze ambaye alionekana kupambana katika kubuni mbinu za kugeuza matokeo hayo ndani ya dakika 90, amesema kwa hakika wachezaji wake walipambana lakini bahati haikuwa kwao.

Amesema hana budi kujiandaa kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, ambao utachezwa mwishoni mwa juma hili Uwanja wa Benjimin Mkapa, Dar es salaam.

“Ni makosa yetu kushindwa kukamilisha mchezo ndani ya kipindi cha kwanza na cha pili kwa kuwa tulipata nafasi tukashindwa kuzitumia hivyo hakuna wa kumlaumu katika hili.”

“Sina budi kujipanga kwa mchezo ujao, nina imani mapungufu yaliyoonekana leo (Jana) nitayafanyia kazi tukiwa kwenye maandalizi kwa siku kadhaa kabla ya kurejea tena uwanjani kupambana na wapinzani wetu wanaokuja.” Amesema Kaze.

Kwa upande wa kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime, amesema wametimiza malengo waliokua wamejiwekea katika mchezo wa jana dhidi ya Young Africans, na ameridhika na matokeo yaliopatikana.

Amesema lengo lao kubwa lilikua ni kupambana na kutoa burudani kwa mashabiki wa soka nchini, na hilo lilitimia tena kwa kikosi chake kupata mabao ya kuongoza, lakini kwa bahati mbaya wapinzani wao walifanikiwa kusawazisha.

“Tuliwekamapengo yetu, kwa hakika ymetimia na ninawapongeza wachezaji wangu kwa kufuata maelezo niowapata kabla na wakati wa mchezo huo ambao mashabiki walifurahia burudani yake.” Amesema Mexime.

Kagera Sugar yenye alama 24 zinazowaweka kwenye nafasi ya 9, itacheza mchezo ujao dhidi ya KMC FC, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Young Africans wanaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 46, baada ya kushhuka dimbani mara 20.

Gomez: Tupo kamili kuwakabili Biashara Utd Mara
Manula, Kakolanya, Salim wamkosha Mbrazil