Uchambuzi wa kitaalam umeonesha kuwa raia watatu wa Venezuela, ambao walikamatwa jijini Nairobi wiki mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, hawakupewa kandarasi na tume ya uchaguzi kama inavyohisiwa, lakini walikuwa na uwezo wa kuzifikia seva za IEBC miezi mitano kabla ya uchaguzi.

Kompyuta zilizokamatwa na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kwa raia hao Salvador Javier, Jose Gregorio na Joel Gustavo unaonyesha kuwa watu hao walikuwa si wafanyakazi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ila walikuwa na fursa ya kufikia taarifa za mawakala.

Hata hivyo, haikuwekwa wazi ikiwa shirika la uchunguzi lingetoa ushahidi, lakini Taifa lilifahamu kuwa DCI ilitaka kuwakamata wageni hao lakini ilizuiliwa na mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ambaye anakabiliwa na changamoto.

Katika mkutano uliofanyika Julai 28, Chebukati aliwahakikishia DCI George Kinoti na Inspekta-Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai kwamba, mifumo ya IEBC haiwezi kupenyeka isipokuwa kwa wafanyakazi walioidhinishwa pekee.

Chebukati pia, alimuambia DCI na IG wakati wa mkutano huo katika ukumbi wa Jogoo House kuwa, Wavenezuela hao watatu walikuwa wamepewa kandarasi na IEBC kutoa usaidizi kwa niaba ya Smartmatic International, kampuni ambayo ilipewa kandarasi ya kutoa teknolojia ya usimamizi wa uchaguzi.

Uchanganuzi kuhusu mifumo ya IEBC na EADH, unaonyesha kuwa kulikuwa na kuhesabiwa kwa matokeo ya urais isivyo halali, ambapo Fomu 34C ilihaririwa mara kadhaa ili kuwiana na fomu 34B na 34A, ambazo ziliingiliwa na kuhaririwa pia.

UNHCR yasifu ukarimu na ulinzi wa Tanzania
Kim Poulsen: Nafasi ya kufuzu CHAN bado ipo