Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametangaza kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na mikusanyiko mikubwa ya watu kwa siku 30 baada ya nchi hiyo kuanza kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Covid 19.

Kenyatta ametoa marufuku hiyo jana Ijumaa Machi 12, 2021 na kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa, marufuku hayo inatekelezwa kikamilifu huku akionya kuwa yeyote atakaye kwenda kinyume, atakamatwa na kufungiliwa mashtaka.

Wiki hii Kenya iliripoti maambukizi makubwa zaidi ya maambukizi ya Corona ambayo ni zaidi ya 800, na kuzua hali ya wasiwasi nchini humo, baada ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuanza kushuhudia kushuka kwa maambukizi hayo mwezi Januari.

Marufuku ya watu kutotembea nje ambayo imekuwa ikiendelea nchini humo tangu mwaka 2020, itaendelea kwa siku zingine 60 kati ya saa nne usiku mpaka saa 10 Alfajiri.

Mbaroni kwa uzushi juu ya afya ya Rais Magufuli
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini yaridhishwa na kasi ya Ujenzi wa JNHPP