Wanawake wanne, Zanzibar wanashikiliwa na polisi kwa kosa la kumsababishia kifo raia wa kijerumani Gerd Winkdl (60), baada ya kumchoma na visu kisa kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Winkdl akiwa na marafiki zake wanne ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, waligombana na baadaye ugomvi huo kusababisha kuchomwa kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Tukio hilo limetokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya Shangani Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 9:30 usiku baada ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2018 akiwa na marafiki zake hao.

Kamanda Ali alisema watuhumiwa hao wanne ambao wote ni wanawake, raia wa Tanzania na Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikiliwa kwa ajili ya kuwahoji na kukamilisha taratibu za kiuchunguzi.

“Inasemekana wote walikuwa wameshalewa na inadaiwa kuwa chanzo cha ugomvi ni wivu wa kimapenzi, lakini tunaendelea na uchunguzi,” Kamanda huyo alisema.

Aidha, Kamanda Ali alibainisha kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mnazimmoja kisiwani hapa.

Rais Museveni awafananisha viongozi wa dini na ‘Kuhani Msaliti’
#Dar24: Waliostahili Tuzo 2017 hawa hapa, Diamond & Ali Kiba wanyukana