Idara ya Jeshi la Polisi ya Memphis nchini Marekani, imekifuta kitengo maalum cha Polisi cha Scorpion, ambacho maafisa wake watano walikuwa wakikitumikia na sasa wapo kizuizini wakituhumiwa kumuua mkazi wa eneo hilo, Tire Nichols (29).

Uamuzi huo, umefanyika baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii ukiwaonyesha maafisa wake watano wakimpiga, Tire Nichols.

Maafisa hao watano, Tadarrius Bean, Demetrius Haley, Desmond Mills Jr, Emmitt Martin III na Justin Smith walifutwa kazi wiki iliyopita na kila mmoja anakabiliwa na mashtaka ya mauaji, unyanyasaji, utekaji nyara uliokithiri, utovu wa nidhamu na ukandamizaji.

Tukio linalodaiwa kufanywa na Scorpion. Picha ya Chigago Sun Times

“Ingawa vitendo viovu vya wachache vinaleta wingu la aibu kwa jina Scorpion, ni muhimu kwamba sisi, Idara ya Polisi ya Memphis, tuchukue hatua za haraka katika mchakato wa uponyaji kwa wote walioathiriwa,” iliongeza.

Hata hivyo Familia ya Nichols ilikaribisha uamuzi huo katika taarifa kutoka kwa mawakili wao, wakisema utafaa na ni wa haki kwa kifo cha kusikitisha cha Tire Nichols, na kusema uamuzi huo ni wa heshima na wa haki kwa raia wote wa Memphis.”

Waandamanaji waliokuwa wakitaka haki ya Tire Nichols Picha ya Gerald Herbert/Associated Press.

Kitengo hicho cha watu 50, kilizinduliwa Oktoba 2021 kwa lengo la kupunguza viwango vya uhalifu katika maeneo fulani korofi, ikiwepo uporaji, wizi wa magari na kwenye maduka makubwa.

Uchunguzi waanza tuhuma wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu
Manzoki avunja ukimya Dar es salaam