Ifikapo mwaka 2020 tarajia kuanza kuona matangazo katika App ya WhatsApp katika sehemu ambayo ‘Status’ huwa zinaonekana, 2018 wamiliki wa WhatsApp na kampuni ya Facebook, walitangaza kuja na mabadiliko kadhaa mojawapo lilikuwa kuhusu matangazo.

Mtandao Facebook ambao kwa sasa ni wamiliki wa App ya WhatsApp  kuanza kufanya majaribio rasmi kipengele hicho kipya katika nchi kadhaa ambazo zina watumiaji wengi wa WhatsApp kama India, Brazil, Marekani na nyinginezo.

Baadhi ya watumiaji hupewa uwezo wa kuona matangazo au kama unatumia App ya WhatsApp ‘Beta’ ambayo ni maalum kwaajili ya kuruhusu majaribio mapya kabla hayajawafikia wengi katika App rasmi.

Aidha maoni yanayotolewa na watumiaji huwapa urahisi wamiliki kuweza kujua madhaifu na kipi waboreshe kabla hawajafanya kuwa rasmi au waamue kuachana nayo.

Takwimu iliyotolewa ya watumiaji wa WhatsApp mpaka sasa  ina zaidi ya watu Milioni 340 duniani, tangu Facebook wainunue mwaka 2014 kwa Dola Bilioni 19 katika makubaliano ambayo yaliwekwa mwanzo, inaelezwa mpango wa kuja kuweka matangazo katika WhatsApp haukuwepo na pia waanzilishi wake walipinga hilo lakini kinachoendelea kwa sasa Facebook wameonesha kukiuka.

Mmoja wa waanzilishi wa WhatsApp Jan Koum, alitangaza kuondoka Facebook mapema mwaka huu huku akiituhumu kampuni hiyo kukiuka makubaliano ambapo udhaifu ulionekana katika mfumo wa ulinzi na kulinda faragha za watumiaji kutokana na skendo iliyowakumba Facebook.

Rais Ramaphosa kuukosa mkutano wa UN
Hapo Kale: Hili ndiyo gari la kwanza kugunduliwa mwaka 1808