Malezi ya Mtoto hutegemea pande mbili za wazazi ili mtoto kukua katika maadili yanayoipedeza jamii na Mungu pia.

Familia nyingi duniani hazijapata baraka hiyo ya kulea watoto kwa pamoja hii inawezekana kwamba baba alimkataa mtoto akiwa tumboni, kufariki kwa mzazi mmoja, wazazi kutengana kwa matatzo yao na ndipo inapotokea swala la malezi ya mzazi mmoja.

Ukiacha katika jamii zinazotuzunguka wapo pia watu maarufu ambao hukutana na changamoto hizi, Nay wa mitego ni mzazi anaefanya malezi peke yake, Ali Kiba, Shamsa Ford, na bidada asiyeisha visa kwenye mitandao ya kijamii Faiza Ally au Mama Sasha Joseph Mbilinyi.

sugu

FaizaFaiza Ally ambaye ni mzazi mwenzake Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (sugu) yeye ameonekana kuwa tofauti na wengine pamoja na kutangaza  mara kwa mara matatizo yake na mzazi mwenzake lakini anaonekana kufurahia malezi ya kuwa (Single mama)

Siku chahe zilizopita katika ukurasa wake wa Instagram Faiza Ally alisema ”nimegundua kuwa single mama ni baraka kubwa sana, zamani niliona ni tatizo kubwa sikukubali na sikutaka kukubali, kiukweli ninampotazama vile Sasha alivyo na furaha naona wazi kabisa maisha yangekua tofauti kama ningeishi na baba yake”.

Mara nyingi Faiza ameonekana mfano wa kuigwa na wanawake wengine, anakufanya usikate tamaa pindi inaotokea umebaki na jukumu la kulea ingawa pia kama mzazi unatakiwa kujua ni njia gani za kulea ili mtoto asiharibike kimawazo kwa kukosa malezi ya mzazi wa upande wa pili.

Bidada huyu asiyeisha vituko kuna kipindi aliangusha party akiwa namuigizaji wa filamu nchini Shamsa Ford wakifurahia maisha ya kuwa single mama’s kama wenyewe wanavyojiita ikiwa bado kulikuwa na madai ya mzazi mwenzake ya kudai kupewa mtoto wake kwani mama yake hana maadili mazuri ya kulea.

Video: Makonda akitangaza kumsimamisha kazi 'Engineer' mkuu wa mkoa wa Dar
Video: 'Top 10' ya Marapa Bilionea na mijengo yao 2016, Majuu