Mashetani Wekundu (Manchester United), wamedhamiria kuibomoa klabu bingwa nchini Italia, Juventus baada ya kuhusishwa na mipango ya kuwa mbioni kumsajili beki Leonardo Bonucci.

Meneja wa Man Utd, Jose Mourinho anatajwa kuwa katika mipango ya kumsajili beki huyo, mara baada ya kukamilisha azma ya kumuhamisha kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba, ambaye tayari dau lake la Euro milion 120 limeshaafikiwa huko Old Trafford.

Taarifa kutoka ndani ya Man Utd, zimethibitisha kuwepo kwa mikakati hiyo kutokana na Mourinho kutoiamini safu yake ya ulinzi, ambayo imekua haifanyia vyema tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson mwaka 2013.

Hata hivyo mpango huo wa usajili wa Bonucci, huenda ukaibua ushindani mkubwa kati ya Man Utd dhidi ya klabu ya Chelsea, ambayo kwa muda sasa imekua ikihusishwa na mikakati ya kutaka kumsajili beki huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Italia kilichoshiriki fainali za Euro 2016 zilizofanyika nchini Ufaransa.

Ujio wa meneja mpya wa Chelsea, Antonio Conte uliibua mipango wa kusajiliwa kwa Bonucci huko Stamford Bridge, kutokana na ukaribu uliopo baina ya wawili hao.

Pep Guardiola: Tutamsajili Leroy Sane
Sam Allardyce Kumrudisha Ulingoni David Moyes