Jina la aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa, jana liliingia tena katika Bunge la Kumi na Moja na kuzua mvutano.

Lowassa alitajwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), wakati akijibu hoja za Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliyekuwa akihoji na kuonesha kushangazwa na uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati alijiuzulu bungeni hapo baada ya kulemewa na kashfa ya akaunti ya ‘Tegeta Escrow’.

Akijibu hoja hizo, Keissy ambaye siku zote ni mbunge mwenye hoja machachari alimvaa Mnyika akifananisha hatua walizochukua wapinzani kwa Lowassa wakati alijiuzulu uwaziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond.

“Mnambeza Muhongo wakati Lowassa alivyojiuzulu hapa hapa bungeni mlichukua mkamtembeza nchi nzima. Leo angekua Rais mgesema nini? Keissy anakaririwa.

Mnyika alikuwa alisoma hatoba ya kambi ya upinzani kwa Wizara ya Nishati na Madini ambayo ilimlenga Profesa Muhongo mara kadhaa.

Polisi yawabana watatu kwa kuvamia na kuua waumini msikitini jijini Mwanza
Video Mpya: Ali Kiba - Aje