Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliungana na msemaji wa CCM, Ole Sendeka pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, katika mazishi ya mbunge wa zamani, Beatrice Shelukindo yaliyofanyika katika kata ya Olorien Jijini Arusha.

Waziri Ummy aliyekuwa muwakilishi wa Serikali katika msiba huo alisema kuwa marehemu Shelukindo amewaachia kumbukumbu isiyosahaulika ya msimamo na ujasiri wake.

Alisema kuwa Shelukindo ambaye hadi anafariki alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), alikuwa imara na jasiri na aliweza kukisimamia kwa dhati kile alichokiamini kuwa kiko sahihi. Pia, alieleza jinsi alivyokuwa mchapakazi na kuusifia utendaji wake katika nyanja za kisiasa.

Lowassa na Ummy Mwalimu

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani, kuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na viongozi wengine wa dini mbalimbali, vyama vya siasa na serikali.

Ibada ya mazishi ilifanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.

Lowassa na NyalanduMsibani

Apumzike kwa Amani. Amina!

Majambazi wadaiwa kuteka kijiji kwa saa kadhaa, Polisi wanena
Serikali yazifungua minyororo ofisi za Mkono