Lupita Nyong’o anadaiwa kushindwa kufanya vizuri katika uhusika wake kwenye filamu ya Star Wars: The Force Awakens.

Muigizaji huyo ambaye alishinda tuzo ya ‘Academy’ kutokana na jinsi alivyofanya vizuri kwenye filamu ya 12 Years A Slave anacheza katika filamu hiyo kama Maz Kanata.

Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti la SUN, muongozaji wa filamu hiyo JJ Abrams hakuridhishwa na jinsi ambavyo Lupita aliigiza uhusika huo kwenye Star Game: The Force Awakens. Inadaiwa kuwa muongozaji huyo alishindwa kuvumilia na kuelekeza Lupita Nyong’o kurudia upya vipande vyake.

Lupita

“Hii huwa inatokea katika kiwanda cha Hollywood, lakini sio jambo la kawaida kwa mshindi wa tuzo kubwa. Nafasi yake katika filamu hiyo huenda ikawa ndogo zaidi,” kilieleza chanzo hicho.

Baadhi ya Watumishi Wa TRA Wakutwa Na Mamilioni Nyumbani Kwao
Wakazi Atajwa Kuwania Tuzo Za KORA 2016