Mamia ya Wananchi nchini Afrika Kusini wameandamana kuendelea kupinga hali ngumu ya maisha na gharama za Maisha.

Maandamano hayo yaliyoenea katika majimbo makubwa zaidi haswa Cape Town na  Pretoria yanaitaka serikali kupunguza gharama za mafuta ikiwemo pia kupunguza kodi ya kwenye mishahara.  

Maandamano hayo yanayoongozwa na Muungano wa vyama vya kibiashara nchini humo ambavyo ni wadau wa wadau wa Chama cha ANC, yana nia ya kupinga ukosefu mkubwa wa ajira, kupanda kwa bei ya mafuta na umeme. 

Maelfu ya wafanyakazi waliingia mitaani katika majimbo yote tisa kudai ruzuku ya msingi ya mapato, kima cha chini cha mshahara bora, na kikomo cha bei ya mafuta na viwango vya riba.

Pia wanataka matatizo yanayoendelea katika kampuni ya usambazaji umeme (ESKOM) inayomilikiwa na serikali yatatuliwe ili wafanyabiashara wasipoteze kazi kutokana na kukatika kwa umeme.

Takribani theluthi ya watu nchini afrika kusini hawana ajira, huku nchi hiyo ikiingia kwenye mzozo wa kiuchumi uliosababishwa na vita ya Ukraine na Russia ikiwemo madhara ya UVIKO 19.
Serikali imesema kuwa inafanyia kazi madai hayo.

Waadamanaji hao ambao waliekea kwenye jengo la Bunge mjini Cape Town wamesema kwamba wataendelea kuandamana mpaka pale watakapopata majibu ya uhakika.

Kipindupindu: 58 wafariki, maambukizi 1,483
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 25, 2022