Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka wadau wa elimu nchini kutoa maoni ya dhati ambayo yatawezesha kufanya maboresho ya sita ya mitalaa ya elimu kuanzia ngazi ya awali, msingi na sekondari.

Akizungumza na wadau wa elimu nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano na wadau mkoani Dar es Salaama Prof. Ndalichako amewasisitiza wadau hao kuelekeza maoni yao katika mfumo utakaowezesha kutoa wahitimu watakaowezesha kufikiwa kwa uchumi wa viwanda.

Aidha, ametahadharisha kuwa, kasi ya kuongezeka kwa wahitimu haiendani na kasi ya nafasi za ajira, hivyo maoni yao yajikite pia katika kutafuta suluhisho la ajira kwa wahitimu nchini, ili waweze kujiajiri na kujitegemea mara wanapotoka vyuoni.

“Taifa lisilo na wahitimu mahiri, kamwe haliwezi kusonga mbele,” amesema Profesa Ndalichako.

Pia Waziri Ndalichako amesisitiza juu ya maoni hayo ambayo pia yanawezwa kuwasilishwa kwa njia ya mtandao kuzingatia mabadiliko ya teknolokjia duniani.

Mabadiliko ya mitaala ambayo yatafanyika sasa yatakuwa ni ya sita tangu uhuru, ambapo mabadiliko ya awali yalifanyika mwaka 1967, 1979, 1997, 2005 na 2014, mabadiliko hayo yote yalilenga kuboresha elimu nchini kuendana na mahitaji ya jamii kwa wakati huo.

Kocha Nabi amkingia kifua Metacha
Jemedari Said: Metacha amekosea sana