Madereva wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) wamepanga kuigomea serikali kwa kile walichodai kuwa wamepewa mikataba mibovu kinyume cha makubaliano yao ya awali.

Madereva hao wameeleza kuwa serikali ilieleza kuwa mshahara wa madereva usipungue shilingi laki nane, lakini walipopata mikataba yao waligundua kuwa wanapaswa kulipwa shilingi laki nne tu.

“Mikataba waliyotupa leo haikidhi yale waliyotuambia leo Mkuu wa VETA alituambia mshahara tutapata shilingi laki nane.  Na juzi Karimjee wadau walisema kwamba mikataba ya madereva mishahara ni shilingi laki nane. lakini leo tumefika hapa mikataba inaonesha mshahara shilingi laki nne, na bonus shilingi laki nne,” alisema Emmanuel Mchape mmoja kati ya madereva wa mabasi hayo.

Alieleza kuwa bonus inaweza kutolewa au isitolewe kulingana na atakavyopenda muajiri. Kadhalika, madereva hao walilalamika kuwa hawakupewa nakala ya mikataba husika.

Chanzo: Kurasa EATV 

Maalim Seif Kutoa Siri ya Mazungumzo ya Kusaka Maridhiano Zanzibar, Leo
Bulembo: Lowassa alitutikisa CCM