Mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli amewanyooshea kidole cha tahadhari wawekezaji waliobinafsishiwa viwanda mjini Iringa lakini wameshindwa kuviendeleza.

Mgombea huyo ambaye ameapa kuwa atashughulika na wawekezaji waliobinafsishiwa viwanda nchini na kushindwa kuviendeleza, amewatahadharisha wawekezaji waliopewa kiwanda cha mjini Iringa kuhakikisha wanakiendeleza kabla ya Oktoba 25, kwa kuwa serikali yake haitawavumilia.

“Wakati nikisoma hapa palikuwa na kiwanda cha National Milling pale, ulikuwa unatengenezwa unga mzuri sana na ulikuwa unasafirishwa mpaka nje. Nimepitapita hapa hicho kiwanda hakifanyi kazi. Inawezekana kimebinafsishwa, inawezekana kuna mtu amekichezea

“Mimi nasema hapa hapa, kama yupo mtu aliyepewa hicho kiwanda na anajua hakifanyi kazi, ahakikishe kinafanya kazi kabla ya tarehe 25 mwezi wa kumi kabla ya hamchagua kwa kura. Akishindwa hivyo, aanze kuandaa documents za kukirudisha,” alisema Dk. Magufuli.

Dk

Dk. Magufuli alifanya mkutano mkubwa wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Iringa Mjini.

 

Video: Lowassa Umemsikia Nape?
Picha: Lowassa Ateka Ngome Nyingine Ya CCM