Mahakama Kuuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora imemtaka aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kulipa kiasi cha shilingi milioni 7.5 kama dhamana.

Jaji wa mahakama hiyo, Leiyla Mgonya alitoa uamuzi huo wa mahakama na kueleza kuwa kiasi hicho cha dhamana ndicho kitakachowezesha kuanza kusikilizwa kwa kesi ya msingi ya kupinga matokeo ya ubunge iliyowasilishwa mahakamani hapo na Kafulila.

Awali, Kafulila aliwasilisha ombi Mahakamani hapo akiitaka mahakama kumpunguzia kiwango cha dhamana kutoka shilingi milioni 15 alizotakiwa kulipa hadi milioni 1 kwa madai kuwa hakuwa na uwezo wa kulipa.

Hata hivyo, Kafulila kupitia kwa wakili wake, Emmanuel Msyani alikubali kulipa kiaisi cha milioni 7.5 kilichoamriwa na mahakama ikiwa ni nusu ya kiwango kilichotajwa awali, hivyo mahakama itaanza kusikiliza kesi yake ya msingi.

Katika kesi yake ya msingi, Kafulila anapinga ushindi wa Hasna Mwilima (CCM).

Ronda Rousey na Holly Holm Kuzichapa Tena
Magaidi Wa IS Watishia Kumuua Papa, Papa Azungumzia Tishio Hilo